Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 727 | Umetazamwa mara 3,711
Download Nota
Kiitikio:
Ona watu wangu wanavyoangamia (vibaya) wanaangamia kwa kukosa maarifa. Wamesahau ya kuwa (mimi ndiye) mwenye maarifa (wamesahau) wamesahau ya kuwa mimi ndiye chanzo cha maarifa.
Mashairi:
1. Kumcha Mwenyezi Mungu ndiyo chanzo cha maarifa, kuzitegemea njia zake kwaongeza hekima, kumcha Mwenyezi Mungu ndiyo chanzo cha maarifa, kumcha Mwenyezi Mungu ndiyo chanzo ha maarifa.
2. Tunaangamia kwa kuwa tumemsahau Mungu,tumesahau njia zake tukafata njia zetu, tukaacha mahusia yake tukafata njia zetu, ndiyo maana tunaangamia kwani tumemsahau Mungu wetu