Ingia / Jisajili

Utenzi Wa Shukrani

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Shukrani | Zaburi

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 2,572 | Umetazamwa mara 8,295

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Mbele ya Miungu, nitaimba zaburi, nitamwimbia Mungu wangu. Nitasujudu, nikilikabili hekalu lako takatifu na kulitukuza jina lako takatifu

Mashairi:

1. Nitakushukuru kwa moyo wangu wote, mbele ya Miungu nitakuimbia zaburi,nitakushukuru kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako Mungu nitakushukuru.

2.Hata siku ile niliyokulilia, ulinijibu Mungu wangu ulinijibu, ukanifariji Ee Mungu ukanifariji, na tena ukanipa nguvu siku ile niliyokuita.

3. Watawala wote watawala wa dunia watakusifu kwa kuimba sifa zako bwana, watakusifu kwa yale ulowatendea, maana utukufu wako ni mkuu juu ya vyote.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa