Mtunzi: Emmanuel Daniel Mutura
> Tazama Nyimbo nyingine za Emmanuel Daniel Mutura
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Emmanuel Daniel Mutura
Umepakuliwa mara 698 | Umetazamwa mara 2,154
Download NotaEE YESU WA EKARISTIA [E.D.MUTURA]
Ee Yesu wa Ekaristia ninakuabudu x2 Umejificha katika maumbo, maumbo ya Mkate na Divai, Ee Yesu wa ekaristia ninakuabudu x2
1. Kwa upendo wako na huruma yako kwetu sisi; umebaki nasi kwa njia ya maumbo ya mkate na divai.
2. Hapo upo mzima Mungu kweli na mtu kweli; watutia nguvu rohoni mwetu nasi tunakuabudu.
3. Tunakuamini na kukuungama; japo hatukuoni kwa macho yetu ila imani yakuona.
4. Mimi nakuamini kwa nguvu zako; unanitakasa Ee Yesu wangu mpenzi wa roho yangu.