Ingia / Jisajili

Bwana Atubariki

Mtunzi: Thomas P. Bingi
> Mfahamu Zaidi Thomas P. Bingi
> Tazama Nyimbo nyingine za Thomas P. Bingi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Thomas Bingi

Umepakuliwa mara 91 | Umetazamwa mara 482

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 27 Mwaka B
- Katikati Dominika ya 6 ya Pasaka Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Bwana atubariki sikuzote,siku zote za maisha yetu ×2.

MASHAIRI.

1.Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake,

Tabu ya mikono yako hakika utaila,utakuwa mwenye heri na baraka tele.

2.Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,Vyumbani mwa nyumba yako,

Wanao kama miche ya mizeituni, wakiizunguka meza yako.

3.Hakika atabarikiwa hivyo yule amchaye Bwana,Bwana akubariki toka sayuni,

Uone uheri wa Yerusalemu, siku zote za maisha yako,

4.Naam ukawaone wana wa wanao,( Amani ikae na Israeli.)Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa