Ingia / Jisajili

Acheni Visingizio

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 2,796 | Umetazamwa mara 5,672

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Wakristo acheni visingizio kwamba hali ngumu, acheni visingizio kwamba hali ngumu x2, (himahima inuka) inuka kitini kitini shika sadaka yako mkononi ulichonacho kwa unyenyekevu kamtolee Muumba wako, kidogo ulichonacho andaa kamtolee Mungu wkao x2.

  • 1.Kwenye sherehe tunatoa michango mikubwa na kanisani , eti tunasema hali ngumu, mtolee Mungu moja ya kumi ya mapato yako naye atafungua milango ya baraka.
  • 2Tunapumua na kuishi kwa neema ya Mungu, ni Mungu ndiye hutuepusha ajali na magonjwa, mtolee Mungu moja ya kumi ya mapato yako naye atafungua milango ya baraka.
  • Tunatumia pesa nyingi kwa anasa za dunia, kumtolea Bwana eti tunasema hali ni ngumu, mtolee Mungu moja ya kumi ya mapato yako, naye atafungua milango ya baraka.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa