Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 580 | Umetazamwa mara 2,111
Download NotaGiza nene limetanda kote kote duniani, limeifunika dunia na hofu yakuzimu imetanda, dhoruba kali inatisha chombo chetu kinazama, mawimbi makali yanakisukasuka nahodha ameshindwa kukiongoza. (Dunia imekuwa kiwanda cha kuzalisha dhambi moshi wake umejaa giza nene lenye sumu kali, inayowaua viumbe wake x2.)
1.Macho yako yamechoka kutazama mambo haya, uzinzi, uchawi na ndoa za jinsia moja, haya ni machukizo, mbele ya uso wako, tumekosa Bwana utuhurumie.
2.Macho yako yamechoka kutazama mambo haya utoaji mimba umekithiri, na kutelekeza watoto majalalani kwa uasherati, haya yote ni giza nene lenye machukizo mbele yako, Bwana utuhurumie.
3.Kwa sababu ya uchu wa madaraka na tamaa ya mali, rushwa, kafara, unyama umezidi watu wanatangatanga hawana imani dunia imejaa magonjwa, vita umaskini wa imani na amani Bwana utuhurumie utuokoe.