Mtunzi: Adolf A. Katambi
> Mfahamu Zaidi Adolf A. Katambi
> Tazama Nyimbo nyingine za Adolf A. Katambi
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: Adolf A. Katambi
Umepakuliwa mara 192 | Umetazamwa mara 474
Download Nota Download MidiAmefufuka ni mzima Aleluya (kweli) Aleluya amefufuka (ni mzima) ameshinda mauti x2
Aleluya amefufuka ni mwokozi wa ulimwengu na mauti haimtawali tena jemedali wa ulimwengu Aleluya amefufuka Aleluya tumshangilie Aleluya amefufuka. x2
MASHAIRI
1. Shangwekuu Yesu kafufuka tumshangilie mkombozi ametukomboa wanadamu ametuletea wokovu amemshinda shetani aleluya amefufuka.
2. Ni mzima kweli kafufuka kaburini hayumo tena na mauti haimtawali Rabi Yesu amefufuka na kaburi liko wazi aleluya amefufuka.
3. Tumetakaswa kwa kifo chake tumetakaswa mioyo yetu tumefaywa wateule wake Mungu Baba yetu wa mbinguni amejitoa sadaka aleluya amefufuka.
4 .Kristo paska wetu kafufuka hafi tena mkombozi wetu Kristo Yesu paska wetu amejitoa sadaka ameyashinda mauti aleluya amefufuka.