Ingia / Jisajili

Ee Baba twakushukuru

Mtunzi: Michael Mgalatia Jelas Nkana
> Tazama Nyimbo nyingine za Michael Mgalatia Jelas Nkana

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Michael Nkana

Umepakuliwa mara 426 | Umetazamwa mara 1,981

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio

//:Ee Baba twakushukuru sana Ee Baba twakushukurusana://

//: Umetulisha chakula toka mbinguni umetunywesha kinywaji toka mbinguni tunakushukuru sana twasema asante://

Mashairi

1.(a) Umetulisha kwa mwili wako chakula cha kiroho baba tunakushukuru tunasema asante,

    (b) Umetunywesha kwa damu yako kinywaji cha kiroho baba tunakushukuru tunasema asante.

2.(a) Mapenzi yako hakika kwetu sisi ni makuu, hata ukajitowa uwe mlo wetu sisi,

    (b) Tunashukuru kwa ukarimu pia kwa wema wako na fadhili zako nyingi zisizo na kipimo.

3.(a) Neema hizo ulizotushushia toka mbinguni ziwe chachu ya kutamani kufika mbinguni,

   (b) Zitukinge na mitego ya adui shetani mwisho tufurahi na wewe milele milele.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa