Ingia / Jisajili

Ee Bwana, naleta Sadaka

Mtunzi: Dr. Charles N. Kasuka
> Mfahamu Zaidi Dr. Charles N. Kasuka
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Charles N. Kasuka

Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 297 | Umetazamwa mara 1,063

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ee Bwana, naleta Sadaka yangu, naomba uipokee, Sadaka ya mtumishi wako, wako mwaminifu x2. {Ni kazi ya Mikono yangu (Bwana), Naomba uipokee Japo ni kidogo sana Mungu wangu nakuomba Ee Bwana Mungu Ipokee x2}.

1.Nafanya kazi kwa juhudi kubwa sababu ya  wema wako, Ee Mungu wangu, sina budi kukutolea, Sadaka kama Asante, Ee Bwana Mungu wangu.

2.Moja ya kumi yakipato changu, Bwana ninakutolea, Ee Mungu wangu, japo ni kidogo sana Mungu wangu nakuomba kipokee, Mungu wangu.

3.Mavuno pia toka Mashambani, nayo ninakutolea, Ee Mungu wangu, ninakutolea kwa Moyo mweupe, nakuomba upokee, Mungu wangu.

4.Sadaka hizi zakukupendeza, Ee Bwana uzipokee, Ee Mungu wangu, kama ulivyoipokea Sadaka ya Abeli Mtumishi, Mungu wangu.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa