Ingia / Jisajili

Ee Bwana Nalikulilia

Mtunzi: Lucas Mlingi
> Mfahamu Zaidi Lucas Mlingi
> Tazama Nyimbo nyingine za Lucas Mlingi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: lucas mlingi

Umepakuliwa mara 1,724 | Umetazamwa mara 3,927

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

EE BWANA NALIKULILIA - BY LUCAS MLINGI

Ee Bwana Mungu wangu nalikulilia ukaniponya x2

1. Ee Bwana nitakutukuza kwa maana umeniinua,

     wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu,

     umeiinua nafsi yngu, Ee Bwana, kutoka kuzimu,

     umenihuisha na kunitoa miongoni mwao washukao shimoni.

2. Mwimbieni Bwana Zaburi, Enyi wataua wake.
    na kufanya shukrani. Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.
    Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,
    katika radhi yake mna uhai. huenda kilio huja kukaa usiku,
    lakini asubuhi huwa furaha. (K)

3. Ee Bwana, usikie, unirehemu,
    Bwana, uwe msaidizi wangu.
    uligeuza matanga yangu kuwa machezo;
    ulinivua gunia, ukanivika furaha
    Ee Bwana, Mungu wangu,
    Nitakushukuru Milele. (K)


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa