Ingia / Jisajili

Ee Nafsi Yangu Umsifu Bwana-I

Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Richard Samson

Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 26 Mwaka C

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ee nafsi yangu, (umsifu) umsifu Bwana, Ee nafsi yangu, umsifu Bwana, Ee nafsi yangu umsifu Bwana x2

1. Bwana huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu walioonewa.
Huwapa wenye njaa chakula,
Bwana hufungua waliofungwa.
2. Bwana huwafumbua macho waliopofuka, Huwainua walioinama.
Bwana huwapenda wenye haki, Huwahifadhi wageni. 
3. Bwana huwategemeza yatima na mjane, Bali njia ya wasio haki huipotosha. Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa