Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Valentine Ndege
Umepakuliwa mara 641 | Umetazamwa mara 1,975
Download Nota Download MidiNitamwimbia Bwana nitamwimbia, kwa maana ametukuka sana x2
1. Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu, naye amekuwa wokovu wangu, yeye ni Mungu wangu nami nitamsifu, ni Mungu wa Baba yangu, nami nitamtukuza.
2. Bwana ni mtu wa vita ndilo jina lake, magari ya Farao na jeshi lake amewatupa amewatupa baharini, maakida yake wamezama katika bahari.
3. Bwana mkono wako wa kuume wawasetaseta adui, kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini, wanao kuondokea wanao kuondokea.