Mtunzi: Alan Mvano
> Mfahamu Zaidi Alan Mvano
> Tazama Nyimbo nyingine za Alan Mvano
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Alan Mvano
Umepakuliwa mara 4,290 | Umetazamwa mara 9,004
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 18 Mwaka C
Kiitikio
( Ingekuwa heri leo muisikie sauti yake ) x2
( Msifanye migumu, msifanye migumu, msifanye migumu mioyo yenu ) x2
Mashairi
1. Njoni tumwimbie Bwana tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu
tuje mbele zake kwa shukrani, tumfanyie shangwe kwa zaburi
2. Njoni tuabudu tusujudu tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba, kwa maana yeye ndiye Mungu wetu
nasi tu watu wa malisho yake na kondoo za mkono wake
3. Msifanye migumu mioyo yenu kama vile huko Meriba, kama siku ile huko Masa jangwani, hapo wazee wenu waliponijaribu
wakanipima wakayaona matendo yangu