Mtunzi: Alan Mvano
> Mfahamu Zaidi Alan Mvano
> Tazama Nyimbo nyingine za Alan Mvano
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Alan Mvano
Umepakuliwa mara 4,182 | Umetazamwa mara 8,681
Download Nota Download MidiKiitikio
Ee Mungu, Ee Bwana Mungu wangu nafsi yangu inakuonea kiu
Mashairi
1. Ee Mungu Mungu wangu nitakutafuta mapema nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku katika nchi kame isiyo na maji
2. Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu, nizione nguvu zako na utukufu wako
maana fadhili zako ni njema kuliko uhai midomo yangu itakusifu
3. Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai, kwa jina lako nitainua mikono yangu
nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono, kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha
4. Maana wewe umekuwa msaada wangu na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia
nafsi yangu imekuandama sana mkono wa kuume unanitegemeza