Ingia / Jisajili

Kaburi Li Wazi

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Wasonga David

Umepakuliwa mara 5,851 | Umetazamwa mara 13,219

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Tukiwa na hofu kubwa, milango imefungwa kwa hofu ya mayahudi, matumaini hatuna ni hofu ndiyo imetutawala, tumekuwa wakiwa kwa kifo chake Kristo msalabani. Tungali tukiwa katika hofu hiyo, hatujui cha kufanya hofu ndiyo imetutawala, tumejifungia ndani kwa hofu ya Mayahudi, tumekata tamaa kwa kuwa Kristo alikufa.

Hata siku ya kwanza ya juma Maria Magdalena na wenzake walikwenda kaburini; wakakuta kaburi li wazi, wakakuta kaburi li wazi hayumo tena, mauti kayashinda katoka mzima kaburini hayumo tena. Wakatuletea habari njema ya ufufuko wa Kristo, tukajawa na matumaini kwani amefufuka, ni kweli amefufuka, ni kweli amefufuka, Bwana wetu kweli ni mzima, mauti kweli ameyashinda, ametoka mzima kaburini hayumo tena.

Ufufuko wa Yesu Kristo umetuletea wokovu, umeimarisha imani yetu, umeimarisha imani yetu, nasi tumekuwa Wakristo kweli katika imani yetu. Ni kweli amefufuka Bwana wetu ni mzima, mauti ameyashinda kamshinda ibilisi, ni kweli amefufuka..............


Maoni - Toa Maoni

Shillah Jul 14, 2022
Iko sawa

Silivano Mar 21, 2022
Upovizuri

Toa Maoni yako hapa