Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,140 | Umetazamwa mara 3,545
Download Nota Download MidiKiitikio:
Mbona mnanisikitisha sana? mbona mnanihuzunisha, mbona mnanifedhehesha enyi viumbe wangu? Mmeyasahau mahusia mmezisahau njia zangu, mmeacha mafundisho yangu mkafata njia zenu, mwanihuzunisha sana mwanifedhehesha sana kwa kuacha mafundisho yangu.
Mashairi:
1.Haya mnayoyafanya si mafundisho yangu, haya mnayoyafanya si mafundisho yangu, kweli mwanisikitisha sana, tena mwanihuzunisha sana tafakarini njia zenu enyi viumbe wangu.
2.Nirudieni, nirudieni, fanyeni toba ya kweli, fanyeni toba ya kweli jipatanisheni na mimi, jipatanisheni na mimi, rejeeni mafundisho yangu niliyowafundisha.