Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 1,785 | Umetazamwa mara 4,974
Download NotaKiitikio:
Twendeni mezani kwa bwana, twendeni sote twendeni, tukale mwili wa bwana, tukanywe na damu yake. Kristo anatualika katika karamu yake, karamu iliyo bora kwa wenye mioyo safi, twendeni sote twendeni tujongee karamuni.
Mashairi:
1.Karamu ya upatanisho yenye neema za Ki-Mungu, Karamu yenye heri na baraka zake Mwenyezi.
2.Karamu iliyoshuka toka mbinguni kwa baba, inayotupatia uzima wa milele.
3. Karamu isiyo na choyo wala fitina za kibinadamu, karamu iliyo ya kweli kwa uzima wa nyoyo zetu.
4. Karamu iliyojaa matumaini ya kweli, karamu yenye kufungua vifungo vyote vya dhambi.