Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 4,435 | Umetazamwa mara 12,456
Download Nota Download MidiKiitikio:
Sala yangu na ipae (mbele zako) kama moshi wa ubani na kuinuliwa kwa mikono yangu iwe kama sadaka ya jioni
Mashairi:
1. Tunakusihi Ee Bwanauipokee sala yetu, ipae mbele yako kama moshi wa ubani iwe kama sadaka ya mtumishi wako Abeli.
2.Matoleo yetu kazi za mikono yetu tunayaleta mbele yako Bwana, kwa unyenyekevu mkubwa twakusihi Ee Bwana uyatakase Ee Bwana twakuomba
3.Vipaji hivi tunavyokutolea vikupendeze Ee Bwana Mungu, vipae mbele yako kama moshi wa ubani, viwe kama sadaka ya jioni