Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 3,402 | Umetazamwa mara 8,093
Download Nota Download Midi
Kiitikio:
Inuka ndugu inuka, ndugu yangu inuka, twende tukamotolee Mungu wetu sehemu ya pato letu. Ee baba e mama inuka twende, Ee kaka e dada inuka twende, twende tukamtolee Mungu wetu sehemu ya pato letu (x2)
Mashairi:
1. Inatupasa kumshukuru kwa yale yote anayotupa, katujalia afya njema inatupasa kumshukuru, twende tukamtolee Mungu wetu sehemu ya pato letu.
2. Ametupa mali nyingi inatupasa kumshukuru, ametupa fedha nyingi inatupasa kumshukuru, twende tukamtolee Mungu wetu sehemu ya pato letu.
3. Mangapi ametupa tena bila gharama yeyote? hivyo nasi tumshukuru kwa yote aliyotujalia.