Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Noeli
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 2,609 | Umetazamwa mara 6,894
Download Nota Download MidiKiitikio:
Leo ni shangwe kubwa chereko nderemo vifijo, leo ni shangwe kubwa kwani mwokozi amezaliwa (x2). Yeye ndiye Mfalme wetu Mfalme Mtukufu, ndiye Mfalme wetu Mtawala wa mbingu na nchi.
Mashairi:
1. Katuletea wokovu ili tupate kuokolewa, kaja kututoa utumwani mwa shetani
2. Yeye ndiye Mfalme wetu Mfalme Mtukufu, ndiye Mtawala Bwana mwenye uweza wa Kifalme.
3. Siku Takatifu imetung'aria leo enyi mataifa njoni tumwabudu Bwana.
4. Gloria, Gloria juu Mbinguni na duniani iwe amani.