Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mwanzo | Zaburi
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 3,323 | Umetazamwa mara 7,901
Download Nota Download MidiKiitikio:
Moyo wangu umekuambia, moyo wangu umekuambia Bwana, Bwana, uso wako nitautafuta, uso wako nitautafuta usinifiche usinifiche, usinifiche uso wako.
Mashairi:
1.Usijiepushe na mtumishi wako kwa hasira, umekuwa msaada wangu, umekuwa msaada wangu, usinitupe wala usiniache, Ee Mungu wa wokovu wangu
2. Baba na mama yangu wameniacha bali Bwana atanikaribisha kwake, Bwana unifundishe njia yako na kuniongoza katika njia iliyonyooka.
3.Kwa sababu yao wanaoniotea, usinitie katika njia ya watesi wangu, maana shahidi, shahidi wa uongo, shahidi wa uongo ameniondokea.
4.Uningoje Ee Bwana uningoje, uwe hodari, uwe hodari, upige moyo konde, Naam uningoje Ee Bwana uningoje.