Ingia / Jisajili

Sikieni Jambo Hili

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 651 | Umetazamwa mara 2,909

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Sikieni jambo hili watu wa dunia tegeni masikio yenu mpate kusikia, mpate kufahamu maneno ya kinywa changu; hebu sikilizeni wakubwa kwa wadogo na jamaa za mataifa, matajiri hata mafukara sikieni jambo hili tegeni masikio yenu.

Mashairi:

1.Maneno ya kinywa changu yatakuwa yenye hekima, maneno ya kinywa changu yatakuwa yenye hekima.

2.Nitatega sikio nipate kufafanua, nipate kufafanua mithali kwa muziki wa zeze

3.Kwanini niogope wakati wa shida, wakati nizungukwapo na uovu wa shetani

4. Watu waovu hutegemea mali zao kwa wingi wa mali zao hujisifiasifia.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa