Ingia / Jisajili

Chimbuko La Imani Yetu

Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: David Wasonga

Umepakuliwa mara 979 | Umetazamwa mara 3,208

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiitikio:

Ufufuko wake Kristo ndiyo chimbuko la Ukristo wetu (x 2). Ufufuko wake Kristo ndiyo asili ya Ukristo; kwakuwa umedhihirisha ushindi dhidi ya mauti, ili kuimarisha imani yetu, tutambue ya kwamba Kristo amefufuka.

Mashairi:

i. Ufufuko wake Kristo ni ushindi dhidi ya mauti, ufufuko wake Kristo ni ushindi dhidi ya shetani, kama siyo kufufuka kwake Kristo imani yetu ingetetereka

ii. Ufufuko wake Kristo umeimarisha imani yetu, ufufuko wake Kristo umeimarisha imani yetu, kama siyo kufufuka kwake Kristo imani yetu ingekuwa haba.


Maoni - Toa Maoni

Daniel Denis Jul 05, 2018
Hongera kwa tungo nzuri ,wimbo huu umenigusa sana ubarikiwe na Mungu aendelee kukupa maarifa zaidi

Toa Maoni yako hapa