Mtunzi: David B. Wasonga
> Mfahamu Zaidi David B. Wasonga
> Tazama Nyimbo nyingine za David B. Wasonga
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Mwaka wa Huruma ya Mungu
Umepakiwa na: David Wasonga
Umepakuliwa mara 3,264 | Umetazamwa mara 11,288
Download Nota Download MidiKiitikio:
Huruma yake Mungu Mwenyezi ni ya milele, huruma yake Mungu Mwenyezi ni ya milele (x2). Mungu wetu ni mwenye huruma, Mungu wetu ni mwenye upendo, huruma yake haibagui wema wala waovu.
Mashairi:
1. Ee Bwana Yesu Kristo ulitufundisha kuwa wenye huruma kama Baba wa Mbinguni.
2.Utuwezeshe sisi wana wako tutambue upendo na huruma yako.
3.Kwa maombezi ya mama Bikira Maria aliye mama wa huruma tuweze kuwa wenye huruma.