Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 785 | Umetazamwa mara 2,132
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Mwanzo Dominika ya 32 Mwaka C
Maombi yangu yafike mbele zako, uutegee ukelele, wangu sikio lako, uutegee ukelele wangu sikio lako ee Bwana x2
1.Ee Bwana Mungu wa wokovu wangu, mchana na usiku nimelia mbele zako
2.Maana nafsi yangu imeshiba tabu na uhai wangu umekaribia kuzimu.
3.Nimehesabiwa nao washukao shimoni nimekuwa kama mtu asiye na msaada.
4.Lakini nimekukimbilia wewe Bwana na asubuhi maombi yangu yatakuwasilia.