Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Ndoa
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 889 | Umetazamwa mara 2,648
Download NotaFamilia kanisa la nyumbani ni shule ya imani na maadili inayofumbatwa katika maisha ya sala, sakramenti za kanisa na Litrujia. Familia ni mahali pamakuzi na elimu makini kwa watoto elimu makini kwa watoto na maendeleo, maendeleo ya jamii jamii zetu. Sote twakili familia ni msingi wa jamii yakibinadamu (na hivyo) familia imara ni kuwa na jamii na kanisa imara.
Dunia imevamiwa na watu wenye agenda ya kugeuza imara na maadili, Wanampangia Mungu atake wanayopanga wanadamu kuwa mema na mabaya. Kwa maombezi ya Bikira Maria Malkia wa Amani. Tupige vita uasi huu ili familia zetu ziwe na upendo, elimu ya dini na kudumisha tunu za maisha ya ndoa. Maandiko matakatifu yanatueleza kazi ya Kristo ili kuwakomboa wanadamu dhidi ya dhambi na matokeo yake mabaya. Hivyo kanisa kama mwili wafumbo wa Kristo, linaendeleza kazi ya Kristo kwa wanadamu kupitia familia. Familia zetu zinakabiliwa na changamoto kama vile talaka ndoa za mitaala, ndoa za jinsia moja, uchumba sugu, ndoa za kurithi wajane, kukosa uaminifu ndani ya ndoa, Familia zisizo na maadili, mchanganyiko wa imani, Familia zisizo na mzazi hata mmoja na familia za mzazi mmoja. Asili ya matatizo hayo ni utamaduni na mazingira na harakati za kila mmoja kuibomoa familia.
Dunia imevamiwa na watu wenye ajenda ya kugeuza imani na maadili, Wanampangia Mungu atake wanayopanga wanadamu kuwa mema na mabaya. Kwa maombezi ya Bikira Maria Malkia wa Amani, tupige vita uasi huu ili familia zetu ziwe na upendo, elimu ya dini na kudumisha tunu za maisha ya ndoa, Ee Baba wa mbinguni tunakuomba utujalie familia imara, kwa kufuata mfano wa familia takatifu ya Nazareti ya Yesu, Maria na Yosefu. Familia zetu ziwe kanisa la awali la nyumbani, shule ya imani matumaini na mapendo, nyumba ya sala na malezi mema kwa wazazi na watoto. AMINA