Maneno ya wimbo
Tunakuomba mama yetu Maria (mwema) teta na mwanao mwanao Yesu
Tunakusihi wewe mama Maria (mama) peleka maombi yetu kwa Yesu.
MABETI
-
Ee Maria nenda kamueleze mwanao, na pia Maria umkumbushe mwanao, alitukomboa kwa damu yake mtini, asikubali apotee mtu, atusaidie.
-
Ee Maria mama mbembeleze mwanao, kwa sauti pole utete nae mwanao, ugumu wa maisha aufute mbali, asikubali shetani ashinde, amuangamize.
-
Mama mpole kwako mwanao utenda, heshima yako kama mzazi hudumu, utakachomwomba atakukirimu, useme yote yatushindayo, ye! atayatenda.
-
Twajua wote tu wasafiri kwa baba, lakini njia tuzipitazo ni ngumu, ombi moja mama atuvushe vyema, shetani atoke mikono tupu, kwa baba tufike.
-
Tunakuumiza kwa dhambi zetu Maria, ila bado wewe ni nguzo yetu Maria, tunahitaji huruma ya kimama, usikubali wanao tuzame, teta na mwanao.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu