Ingia / Jisajili

Tuwaheshimu Baba Na Mama

Mtunzi: John William Kasole (Joka)
> Tazama Nyimbo nyingine za John William Kasole (Joka)

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Gervis Kasole

Umepakuliwa mara 1,374 | Umetazamwa mara 4,817

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Tuwaheshimu baba na mama, tuwaombee maisha mema, ndivyo inavyosema sheria tutabarikiwa (na)

Wanapopoteza ufahamu, katu tusije wakaripia, tuwalee tuwatunze vyema tutabarikiwa.

Walitulea walitutunza walitufundisha yote mema, japo tuliwakosea sana hawakutuchoka

Walitulisha walitunywesha walituvisha walitulaza, tu-wapende wazazi wetu tutabarikiwa.

MABETI

1. Waheshimu bila kuchoka uwapende bila kikomo, wafanyie kila kilicho chema cha kupendeza

     Kua mwanga pachoni pao, kua nuru moyoni mwao, kua cheko nyusoni mwao kua pumziko lao.

2. Kero nyingi walizipata katika kutulea sisi, walivumilia mengi katika malezi yetu

   Asubuhi hawakuchoka mchana hawakutuacha, usiku hawakulala ili tupate amani.

3. Katu tusiwahuzunishe na katu tusiwasikitishe, ongea nao kwa upole na kwa unyenyekevu

   Cheko lao baraka kwako na raha yao neema kwako, lililo jema kwa wazazi ni baraka kwa mwana.

4. Tuwapende wazazi wetu  tuwapende wazazi wetu, tuwapende wazazi tuwapende wazazi wetu

   Waheshimu wazazi wako waheshimu wazazi wako, utaheshimiwa na wanao kweli na wanao.

Copied By Gervis Kasole


Maoni - Toa Maoni

Zuchu Mar 26, 2024
Nawapenda sana

Toa Maoni yako hapa