Ingia / Jisajili

Muonekano Wa Siku

Mtunzi: John William Kasole (Joka)
> Tazama Nyimbo nyingine za John William Kasole (Joka)

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: frank moses

Umepakuliwa mara 277 | Umetazamwa mara 1,224

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Uamkapo asubuhi kumbuka kumshukuru MUNGU, unapofanya kazi zako usisahau kumu-omba

Utembeapo mtukuze kwa uhai ulio nao, unapolala kitandani usisahau kumuomba, mpe MUNGU uhai wako atawale

Ufanye kazi siku sita ya saba nenda kamuabudu, ukamtolee sadaka kipato chako kitazidishwa, usilisahau agano la Mwenyezi

MABETI

  1. Unaamka tu kwa neema, wapumua tu kwa rehema, yafanye maisha yako kwa mapenzi yake.
  2. Unatembea kwa hisani, unapumua bure bure, neno asante kwa MUNGU kinywa kitamke.
  3. Unapofanya kazi zako na upumzishavyo mwilio, pozo tosha ni kwa MUNGU muweza wa yote.
  4. Unapolaza mwili wako, unapofumba macho yako, twaamka kwa neema tumuombe MUNGU.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa