Ingia / Jisajili

Mtajuta

Mtunzi: John William Kasole (Joka)
> Tazama Nyimbo nyingine za John William Kasole (Joka)

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: frank moses

Umepakuliwa mara 494 | Umetazamwa mara 1,548

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ee baba Ee mama sina hatia, uhai ni tunu toka kwa MUNGU, mnaniua bure, (kwake MUNGU(chozi laana))Mtajuta

MABETI

  1. Ni mpango wa MUNGU mimi niishi lakini kwa ukali waniua
  2. Kosa langu ni nini mimi kichanga, sumu kali tumboni mwaninywesha.
  3. MUNGU kanipa pumzi niweze ishi, ya nini mwanadamu uniue.
  4. Daktari MUNGU kakupa ufahamu, wa kuponya wala si wa kuua.
  5. Ole wako mama unaeniua, aheri mgumba asiyezaa
  6. Uchungu wa sumu uninyweshayo nife, utakua na maisha machungu.
  7. Nimekukosea nini wewe baba, hata umwache mama aniue.
  8. Nionee huruma nami niishi, nione japo mwezi nalo jua
  9. Kosa lenu baba mama na daktari, kwa MWENYEZI hukumu yawangoja.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa