Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki
Makundi Nyimbo: Noeli
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 418 | Umetazamwa mara 1,812
Download Nota Download MidiMASIHA AJAYE
@Martin Munywoki
U T A N G U L I Z I
Je, wewe ndiwe Masiha (ndiwe yule) yule tunayemtarajia,
(Wewe) Je, wewe ndiwe ujaye (na nguvu) mwenye uweza kutukomboa?
Je, wewe ndiwe Masiha (ndiwe yule) yule waliyetuahidia,
(Au) Je, bado yupo mwingine (ajaye) tupaswaye kungojea?
K I I T I K I O
sop / alto
{ Umekuja, kwetu mpole kabisa,
Umevua, utukufu nguvu fahari,
Kajivika, ubinadamu kabisa,
Umekuja, ulimwenguni dhaifu,
Makusudi, wewe utuokoe sisi } *2
tenor/bass
{ Umekuja mtoto, u mpole kabisa,
Na umevua ukuu, utukufu fahari,
Ukajivika unyonge, wa mwanadamu kabisa,
Na umekuja tuliko, tungali dhaifu,
Kwa makusudi, wewe utuokoe sisi } *2
M A S H A I R I
1. Leo limetimia, lile andiko la manabii,
Kwamba bikira atachukua mimba,
Na kumzaa mtoto wa kiume, na kumuita Emanueli!
2. Amejishusha mno, humu pangoni Betilehemu,
Alimolala mchanga na mnyonge,
Kusudi tumfikie bila woga, nani amuogopaye mtoto?
3. Wachungaji kondeni, na mamajusi wa mashariki,
Na watu wa pande zote za dunia,
Wakusanyika wanamsogelea, wote wamsujudia mtoto!