HAKI YETU
Haki yetu (haki yetu) *2 haki yetu (wachanga) iko wapi * 2
1. Nimekulilia usiku na mchana (mama), utege sikio lako unisikie (mama)
Uniruhusu nifike duniani, usininyime haki ya kuzaliwa (mama)
Usiniavye ningali mimba, na mimi pia ni binadamu
2. Hata usiponizaa we mama yangu (mama), ujue nakupenda na sina mwingine (mama)
Nitazaliwa na nani ila wewe, na mimi ni baraka yako kutoka (juu)
Na sitakusahau milele, na utanikumbuka milele!
3. Kwa nini unajipenda we mama yangu (mama), unaona aibu unaponibeba (mama)
Hauna huruma kwangu mi mwanao, unawaua wachanga kwa makemikali
Wengine unatupa chooni, na hao pia binadamu!
4. Wewe usingezaliwa we mama yangu (mama), ungetoka wapi huko ulimwenguni (mama)
Wala haungetimiza ndoto zako, na kuijua dunia wala raha (zake),
Mbona hutaki nami niishi, na mimi pia ni binadamu