Mtunzi: Martin Mutua Munywoki
> Tazama Nyimbo nyingine za Martin Mutua Munywoki
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Eusebius Joseph Mikongoti
Umepakuliwa mara 560 | Umetazamwa mara 2,699
Download Nota Download MidiTENDA WEMA
1. Mara kwa mara wanadamu ni wagumu sana, Hawajali wajipenda tu, hata hivyo uwasamehe wasamehe
{Tenda wema usichoke tenda wema nenda zako
(tazama) hii dunia hailipi (lakini) tenda wema (kwa watu) } *2
2.Ukiwa mkarimu watu watakushutumu, Watasema u mnafiki, hata hivyo endelea kuwa mwe-ma
3. Unapokuwa mwaminifu na mkweli kwao, Wanaweza kukudanganya, hata hivyo usiache kuwa mkweli
4.Ukiwa nao utulivu, ukifurahiya Baadhi wataona wivu, hata hivyo endelea kufurahia
5. Mema uyatendayo leo, mema utendayo, Kesho yatasahaulika, hata hivyo usichoke kutenda wema
6.Hata ukijitoa kwao kwa uwezo wote, Bado ha-wataridhika, hata hivyo jitolee kwa moyo wote
7. Kwa maana tazama hatima ya haya yote, Ni baina yako na Mungu, hata hivyo si baina yako na wao