Mtunzi: Kennedy Mulwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Kennedy Mulwa
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: Kennedy Mulwa
Umepakuliwa mara 5 | Umetazamwa mara 5
Download NotaUTUHURUMIE
Utuhurumie, utuhurumie,
utuhurumie, utuhurumie
(Bwana, Bwana, bwana, utuhurumie)
Utuhurumie, utuhurumie, utuhurumie,
utuhurumie
(Kristu, Kristu, Kristu, utuhurumie)
Utuhurumie, utuhurumie, utuhurumie,
utuhurumie
(Bwana, Bwana, bwana, utuhurumie)
UTUKUFU
Utukufu kwa Mungu juu mbinguni
Na amani duniani, kwao aliowaridhia x2
1. Tunakusifu, tunakuheshimu, twakuabudu, tunakutukuza;
twakushukuru Mungu kwa ajili ya utukufu wako mkuu.
2. Ee Bwana Mungu, mfalme wa mbinguni, Baba Mwenyezi Muumba wa vyote;
Ee Bwana Yesu mwana wa pekee, mwanakondoo, mwana wake Baba.
3. Uondoaye dhambi za dunia, tuhurumie, utuhurumie;
Uondoaye dhambi za dunia, ulipokee hili ombi letu.
4. Unayeketi kuume kwa Baba, tuhurumie, utuhurumie;
Kwa kuwa wewe ndiwe peke yako, Mtakatifu, peke yako Bwana.
5. Pekee yako mkuu Yesu Kristu, pamoja naye Roho Mtakatifu;
Kwa utukufu wake Mungu Baba, milele yote, amina, amina
ALELUYA
MTAKATIFU
Mtakatifu,
mtakatifu, mtakatifu
Bwana Mungu,
(Mungu) wa majeshi
Mtakatifu,
mtakatifu, mtakatifu
Bwana Mungu,
(Bwana Mungu) wa majeshi
Mbingu na
dunia zimejaa utukufu,
Zimejaa utukufu wako mkuu
Hosana,
hosana juu mbinguni,
Hosana, hosana juu mbinguni.
M’barikiwa
‘nayekuja kwa jina la Bwana,
M’barikiwa ‘nayekuja kwa jina la Bwana.
Hosana…
AMINA
MWANAKONDOO
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za ulimwengu,
(U)tuhurumie, tuhurumie
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za ulimwengu,
(U)tuhurumie, tuhurumie
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za ulimwengu,
Utujalie amani;
Utujalie amani.