Mtunzi: Kennedy Mulwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Kennedy Mulwa
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: Kennedy Mulwa
Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0
Download NotaMISA VERONIKA
UTUHURUMIE
Ewe Bwana
tuhurumie
Ewe Kristu
tuhurumie
Ewe Bwana
tuhurumie
UTUKUFU
T: Utukufu
kwa Mungu juu mbinguni
W: Na amani
duniani kwao watu aliowaridhia
(Bwana) Tunakusifu, tunakuheshimu, tunakuabudu
(Bwana), tunakutukuza x2
1. Baba tunakushukuru, kwa ajili ya
utukufu wako
2. Ewe Mungu ni mfalme, wa mbinguni,
Mungu Baba Mwenyezi
3. Bwana Mungu mwanakondoo, wake Mungu ni
mwana wake Baba
4. Ewe mwenye kuziondoa, dhambi za dunia
tuhurumie
5. Ewe mwenye kuketi kuume, kwake Mungu
Baba, tuhurumie
6. Pekee yako Mtakatifu, pekee yako ni
Bwana Yesu Kristu
7. Naye
Roho Mtakatifu, katika utukufu wake Baba
MTAKATIFU
Mtakatifu
x3 Bwana Mungu
Mtakatifu
x3 wa majeshi
Mbingu na
dunia zimejaa utukufu wako Ewe Bwana Mungu
Hosana juu, Hosana juu, Hosana juu mbinguni
(Hosana)
Hosana juu, Hosana juu, Hosana juu mbinguni
Mbarikiwa
ni yule ajaye kwa jina lake Bwana x2
Hosana...
BABA YETU
Baba yetu wa mbinguni, jina lako litukuzwe
1. ‘falme wako uje kwetu, utakalo
lifanyike, duniani kama mbinguni.
2. Tupe leo
mkate wetu, mkate wetu wa kila siku, utakalo lifanyike.
3. Tusamehe
dhambi zetu, kama vile twawasamehe, nao waliotukosea.
4. Situtie
majaribuni, maovuni utuopoe, utakalo lifanyike.
5. Kwa kuwa
‘falme ni wako, nazo nguvu na utukufu, vyote vyako hata milele.
MWANAKONDOO
{Mwanakondoo
wa Mungu ee
(Ee Mwana)
Ee Mwana, (kondoo) wa Mungu}
Uondoaye
dhambi zetu tunakuomba utuhurumie
{Mwanakondoo
wa Mungu ee
(Ee Mwana)
Ee Mwana, (B: kondoo) wa Mungu}
Uondoaye
dhambi za ulimwengu tunakuomba utuhurumie
{Mwanakondoo
wa Mungu ee
(Ee Mwana)
Ee Mwana, (B: kondoo) wa Mungu}
Uondoaye
dhambi za ulimwengu tunakuomba utupe amani