Mtunzi: Kennedy Mulwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Kennedy Mulwa
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: Kennedy Mulwa
Umepakuliwa mara 8 | Umetazamwa mara 7
Download NotaMISA CHAVARA
UTUHURUMIE
Ewe Bwana, ewe Bwana, ewe Bwana tuhurumie
(Ewe) Bwana tuhurumie (ewe) Bwana tuhurumie
Ewe Kristu, ewe Kristu, ewe Kristu
tuhurumie
(Ewe) Kristu tuhurumie (ewe) Kristu
tuhurumie
Ewe Bwana, ewe Bwana, ewe Bwana tuhurumie
(Ewe) Bwana tuhurumie (ewe) Bwana tuhurumie
UTUKUFU
Utukufu kwa Mungu mbinguni
Na amani kote duniani, kwao wenye
aliowaridhia
1.
Tunakusifu, tunakuheshimu,
twakuabudu, tunakutukuza; twakushukuru Mungu kwa ajili ya utukufu wako mkuu.
2.
Ee Bwana Mungu, mfalme wa
mbinguni, Baba Mwenyezi Muumba wa vyote; Ee Bwana Yesu mwana wa pekee,
mwanakondoo, mwana wake Baba.
3.
Uondoaye dhambi za dunia,
tuhurumie, utuhurumie; uondoaye dhambi za dunia, ulipokee hili ombi letu.
4.
Unayeketi kuume kwa Baba,
tuhurumie, utuhurumie; Kwa kuwa wewe ndiwe peke yako, Mtakatifu, peke yako
Bwana.
5.
Pekee yako mkuu Yesu Kristu,
pamoja naye Roho Mtakatifu; Kwa utukufu wake Mungu Baba, milele yote, amina,
amina
MTAKATIFU
Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu Bwana Mungu
Mtakatifu Bwana Mungu, Bwana Mungu wa
majeshi
Mbingu na dunia zote zimejaa utukufu wako
Zimejaa utukufu, utukufu wako ee Bwana
Hosana, hosana, hosana juu mbinguni
Hosana, hosana, hosana juu mbinguni
Mbarikiwa, mbarikiwa ni ajaye kwa jina la
Bwana
Mbarikiwa ni ajaye, ni ajaye kwa jina la
Bwana
Hosana…
MWANAKONDOO
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za
ulimwengu,
Tuhurumie, utuhurumie
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za
ulimwengu,
Tuhurumie, utuhurumie
Mwanakondoo wa Mungu, uondoaye dhambi za
ulimwengu,
Utujalie amani