Ingia / Jisajili

Mungu Atakujibu

Mtunzi: Alvin Marie
> Mfahamu Zaidi Alvin Marie
> Tazama Nyimbo nyingine za Alvin Marie

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Alvin Marie

Umepakuliwa mara 26 | Umetazamwa mara 35

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Bwana Mungu wako aliyekukomboa asema, usifadhaike na tena usiogope. Yeye si kipofu asiweze kuona hitaji, wala si kiziwi akose kukusikia. Anajua shida zako, anajua mateso yako. afahamu ombi lako, anaona hitaji lako. kwa wakati wake Mungu hakika atakujibu. x2 2. Shida za maisha, mizigo mingi yakulemea, umefika mwisho huoni matumaini. Umepungukiwa maisha yamekuwa magumu, usivunjike Moyo mwenyexi yuko na wewe. 3. Kwenye maji mengi asema atakuwa na wewe, hata kwenye moto hakika hatakuacha. Ndugu na rafiki wakikutenga na kukimbia, mkombilie Mungu hashindwi jambo lolote

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa