Maneno ya wimbo
MUNGU UNIHIFADHI MIMI KWA MAANA NAKUKIMBILIA WEWE
Mungu, unihifadhi mimi*2
Kwa maana nakukimbilia Wewe *2
1. Bwana ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu. Nimemweka Bwana mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuumeni kwangu, sitaondoshwa
2. Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini. Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.
3. Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu