Ingia / Jisajili

Shangwe za Pasaka

Mtunzi: Valentine Ndege
> Mfahamu Zaidi Valentine Ndege
> Tazama Nyimbo nyingine za Valentine Ndege

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Mika Wihuba

Umepakuliwa mara 2,784 | Umetazamwa mara 5,728

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Shangwe, shangwe, shangwe, shangwe Leo ni shangwe Bwana Yesu kafufuka, shangwe shangwe shangwe shangwe Leo ni shangwe Bwana Yesu kafufuka Kaburi liwazi Bwana hayumo kashinda mauti Yesu kafufuka hebu tazameni mlipomweka yuko Galilaya ndiko mtamwona.

1.Kimya kuzimu, mbinguni shangwe, shetani nikimya, mbinguni ni raha, ametukomboa utumwa wa shetani.

2.Simba wa Yuda anaunguruma, wanyama mwituni wamekimbia, simba huyu ni Yesu kafufuka yu mzima.

Hitimisho.

(Watu wote simameni kwa furaha shangilia) Mwokozi wetu amefufuka Aleluya (Watu wote simameni kwa furaha, shangilia) Mwokozi wetu amefufuka Aleleuya, (watu wote) piga makofi (nakuimba) piga makofi (nakucheza) piga makofi (midundo) piga makofi (piga miluzi leo ni shangwe) shangilia (ngoma zipigwe kinanda kichezwe) shangilia. Ni raha, ni raha ni shangwe, ni shangwe. Shangwe za Paska.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa