Maneno ya wimbo
NALIFURAHI WALIPONIAMBIA
Nalifurahi waliponiambia, nalifurahi waliponiambia na twende nyumbani, nalifurahi waliponiambia na twende nyumbani mwa Bwana*2
1. Nalifurahi waliponiambia na twende nyumbani mwa Bwana miguu yetu imesimama ndani ya malango yako ee Yerusalemu
2. Ee Yerusalemu ulijengwaa kwa mji u lioshikamana, huko ndiko walipopanda panda kabila, kabila za Bwana
3. Ushuhuda kwa Israeli walishukuru jina la Bwana, maana huko viliwekwa viti vya hukumu, viti vya enzi vya mbari ya Daudi
4. Kwa ajili ya ndugu zangu na rafili zangu, niseme sasa, amani ikae nawe, kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu, nikutafutie nikutafutie mema
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu