Mtunzi: Adolf A. Katambi
> Mfahamu Zaidi Adolf A. Katambi
> Tazama Nyimbo nyingine za Adolf A. Katambi
Makundi Nyimbo: Misa
Umepakiwa na: Adolf A. Katambi
Umepakuliwa mara 133 | Umetazamwa mara 348
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 6 Mwaka A
Ndiwe sitara yangu Ee Bwana utanihifadhi na mateso (mateso) utanihifadhi na mateso. x 2
Utanizungusha utanizungusha utanizungusha nyimbo za wokovu nyimbo za wokovu nyimbo za wokovu utanizungusha nyimbo za wokovu. x 2
MASHAIRI
1. Heri aliyesamehewa, dhambi na kusitiriwa makosa. Heri Bwana asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake ambaye rohoni mwake hamna kitu.
2. Nalikujulisha dhambi yangu, wala sikuuficha upotovu wangu. Nalisema nitayakiri maasi yangu kwa Bwana, nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi wa dhambi yangu.
3. Mfurahieni Bwana, Shangilieni enyi wenye haki. Pigeni vigelegele enyi wenye haki, ninyi nyote mlio wanyofu enyi nyote mlio wa nyofu wa moyo.