Ingia / Jisajili

Nikufanye Rafiki

Mtunzi: Erick Mwaniki
> Tazama Nyimbo nyingine za Erick Mwaniki

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari | Shukrani

Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata

Umepakuliwa mara 78 | Umetazamwa mara 503

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
NIKUFANYE RAFIKI 1. Kuna mambo mi' natakanikujuze yapo mengi ninahisi nikuambie kuhusu yaliyomo maishani mwangu, nisimulie maana wategasikio, kama rafiki rafiki mwaminifu Wewe wanijua, unanifahamu, unanielewa, umenichunguza, Wanisikiliza, unanishauri, unanisamehe, wewe ni rafiki hivyo naomba nikufanye, rafiki yangu mwema, rafiki mwaminifu wewe uliyekamilika, nikamilishe mimi, kwa pendo lako wewe 2. Nimekumbwa nayo masaibu tele, kajipata naegemeaya dunia, nayo kanipotosha kaniangamiza, yakanifumba macho sikuoni tena lakini wewe ukanihurumia 3. Nilidhani raha ndiyo kila kitu, mle ndani niliona kwamba 'kafika, sheria yako nayo sikuifuata, na pia yote yale ulonifundisha, na bado utayari kunisamehe 4. Nikaona yote kawaida kwangu, afya njema lishe bora pia furaha, ni kwa neema zako nimefanikiwa, kuishi vema pia kuyaona mema, na hayo yote niwe wanijalia

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa