Mtunzi: Reuben Maghembe
> Tazama Nyimbo nyingine za Reuben Maghembe
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Reuben Maghembe
Umepakuliwa mara 1,129 | Umetazamwa mara 3,225
Download Nota Download MidiKiitikio
Nikushukuruje ewe Mungu wa wokovu wangu *2
Asante kwa uzima na kwa ulinzi wako
Asante kwa huruma na kwa rehema zako
Sina chochote cha kukulipa bali nasema asante
Beti
1. 1. Katika haya maisha yangu nimepita magumu mengi lakini yote
kwa neema yako nimeyashinda ee Mungu nikushukuru nikushukuruje kwa wema wako
2. 2. Niamkapo na nilalapo ni kwa wema wako Mungu si kwa
uwezo wangu ni fadhila zako na upendo wako sina budi kukushukuru ee Mungu wangu
3. 3. Kila uchao na uchwao ni majanga nazo ajali lakini kwa
upendo wako unanivusha salama si kwa sababu mimi mwema ni huruma yako
4. 4. Mafanikio niliyonayo si wote wameyapata si kwa kuwa
mimi ni bora ni fadhila zako sina budi kukushukuru ee Mungu wangu