Mtunzi: Reuben Maghembe
> Tazama Nyimbo nyingine za Reuben Maghembe
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Kwaresma | Ubatizo
Umepakiwa na: Reuben Maghembe
Umepakuliwa mara 469 | Umetazamwa mara 2,257
Download Nota Download MidiKiitikio: Bwana nitakutafuta Bwana nitakutafuta Ee Bwana nitakutafuta Ee Bwana, maana u ngome yangu wewe ndiwe wokovu wangu *2
Mchana kutwa na usiku kucha nitakutafuta Ee Bwana, Usijifiche nikutafutapo Ee Mungu wawokovu wangu
Kwani we we ndiwe kinga yango kimbilio langu na msaada wangu.
Mashairi
1. Moyo wangu umekuambia Bwana uso wako uso wako nitautafuta, nitautafuta usinifiche uso wako.
2. Umekuwa msaada wangu msaada wangu siku zote siku zote za maisha yangu, wala usinitupe nikutafutapo Ee Mungu wangu
3. Mahali pako Ee Bwana ni mahali patakatifu na pa wokovu na utakaso wa nafsi yangu, nikaribishe Ee Mungu wangu katika maskani yako
4. Matatizo mengi ya dunia hii yananizonga sana natapatapa na nafsi yangu ninakimbilia kwako nipokee Ewe Mungu wangu