Ingia / Jisajili

Nimekuja Kuyafanya Mapenzi Yako

Mtunzi: John Mgandu
> Tazama Nyimbo nyingine za John Mgandu

Makundi Nyimbo: Mwanzo | Zaburi

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 19,987 | Umetazamwa mara 30,271

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ndipo niliposema, tazama nimekuja Bwana nimekuja, tazama nimekuja kuyafanya mapenzi yako x 2

  1. Nalimngoja Bwana kwa saburi, akaniinamia akakisikia kilio changu, akatia wimbo mpya kinywani mwangu ndiye sifa zake Mungu wetu.
     
  2. Dhabihu na matoleo hukupendezwa nayo, masikio yangu umeyazibua, kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka, ndipo niliposema tazama nimekuja.
     
  3. Katika gombo la chuo nimeandikiwa, kuyafanya mapenzi yako, mapenzi yako, ee Mungu wangu ndiyo furaha furaha yangu, naam sheria yako i moyoni mwangu.
     
  4. Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kusanyiko kubwa, sikuizuia midogo yangu, ee Bwana, ee Bwana, ee Bwana unajua. 

Maoni - Toa Maoni

Simon Shimba Jan 14, 2021
siku hizi kuna usahihishaji wa kila nyimbo za zamani zilizotungwa na legend kama Mgandu kila nyimbo zilizoko swahili wanasema zinamakosa wanaoziapload wanaweka tungo zenye makosa ?

Emanuel Jan 10, 2018
Mabeti yawimbo yamekosewa hayafanani na yaawali Napenda kujua kama ulifanyiwa marekebisho au tayping error?

Toa Maoni yako hapa