Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Bernard Mukasa
Umepakuliwa mara 37,271 | Umetazamwa mara 55,072
Download NotaKIITIKIO:
Niseme nini Ee Bwana? Nitamke maneno gani kinywani? Nikushuru jinsi gani?
Nisimulie vipi mimi, mapito niliyopita kuja hapa? Nikutukuze vipi Mungu?
Niseme tu (Bwana) Mungu (wangu); asante nakushukuru. Narudia (Bwana) Mungu (wangu); Asante nakushukuru.
1. Nakumbuka nilivyojaribu; Sikujua kama utajibu; nikapapasa mkono gizani, kulipokucha ni tunda mkononi.
2. Katikati ya safari maji yote yakamwagika chini. Lakini kwa wema wako ukayazoa yakajaa upya.
3. Nilipigwa mawe, nikaaibishwa mimi, tazama leo umeniona; ukamtukuza mtumishi wako.