Mtunzi: Reuben Maghembe
> Tazama Nyimbo nyingine za Reuben Maghembe
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Miito | Shukrani
Umepakiwa na: Reuben Maghembe
Umepakuliwa mara 595 | Umetazamwa mara 2,263
Download Nota Download MidiKiitikio
Nimetafakari matendo yako ee Mungu
wangu Nimeitikia na wito wako Ee Mungu wangu
Nimeisikia sauti yako Mungu Ninakuja
kwako unipokee Mungu wangu
Nimezikumbuka rehema zako Ee Mungu
wangu
Bwana niwe wako nikaribishe nyumbani
mwako*2 katika himaya ya Bwana mimi nifanye makazi na Bwana nitazitangaza rehema
zako Ee Mungu wangu
katika himaya ya Bwana mimi nifanye
makazi na Bwana nitazitangaza rehema zako Bwana Mungu wangu
Mashairi
1.
Naja kwako unifanye mtumwa wako,
unibariki Bwana unifanye chombo cha amani unitakase palipo na chuki nipande
mbegu ya upendo wako Bwana
2.
Niwe wako Bwana unitume niende mimi Bwana
unishike mkono nikawapake mafuta yako Bwana nijalie Roho wako aniongoze katika
kazi yako Ee Bwana
3.
Ninayo furaha kuja mbele zako Ee Mungu
niwe miongoni mwao wakupendezao na niwe kati yao waienezao Injili.