Ingia / Jisajili

Njoni Twimbe (Pasaka)

Mtunzi: Reuben Maghembe
> Tazama Nyimbo nyingine za Reuben Maghembe

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Reuben Maghembe

Umepakuliwa mara 1,313 | Umetazamwa mara 4,801

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Kiikitio:

Njoni twimbe leo njoni twimbe kwa furaha watu wote njoni twimbe kwa furaha tumsifu Mwokozi x 2

Ni shangwe chereko cheroko leo pia nderemo navyo vifijo kwani Mwokozi amefufuka, Watu wote leo njoni tufanye sherehe sote tufurahi tumsifu Mwokozi kashinda mauti x 2

Beti:

1. Enyi matifa njooni tufanye shangwe, Mkombozi wetu kashinda mauti sasa ni mzima mzima mzima, kaburini sasa haumo hayumo, aleluya njoni sote tumshangilie. Na ngoma na vinanda tupige tucheze tushangilie

2. Makanisa yote yaimbe kushangilia, ukombozi wetu umeonekana sasa si huzuni tena ni furaha, aleluya twimbe nyimbo za furaha, Waumini wote simameni kwa furaha. Kengele za kanisa zipigwe kuashiria ushindi.

3. Dunia yote inaimba kushangilia, ufufuko wake mshinda mauti kafufuka kama alivyosema, sasa hafi tena kamwe hafi tena, aleluya twimbe aleluya aleluya. Na ngoma na vinanda tupige tucheze tushangilie.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa