Mtunzi: Emmanuel Daniel Mutura
> Tazama Nyimbo nyingine za Emmanuel Daniel Mutura
Makundi Nyimbo: Mazishi
Umepakiwa na: Emmanuel Daniel Mutura
Umepakuliwa mara 499 | Umetazamwa mara 2,300
Download NotaTULIVYO SASA NDIVYO ALIVYOKUWA (E.D.MUTURA)
(TAFAKURI YA FUMBO LA KIFO)
Tulivyo sasa ndivyo alivyokuwa (marehemu) na alivyo sasa ndivyo tutakavyokuwa (sisi) tumuombe Mungu atujalie tufe kifo chema x2
1. Tuchunguze mwenendo wa maisha yetu, tuyatende yampendezayo Mungu wetu siku za uhai wetu.
2. Twaamini ya kwamba kwa kifo cha mwili, tunafunguliwa mlango wa maisha mapya maisha ya milele.
3. Basi sisi tukeshe kila wakati, kwani hatujui ni siku ipi Bwana wetu atatwita kwake.
4. Tukumbuke kujipatanisha na Mungu, kwa kuziungama dhambi zetu zote ili tufike mbinguni.