Mtunzi: Emmanuel Daniel Mutura
> Tazama Nyimbo nyingine za Emmanuel Daniel Mutura
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Emmanuel Daniel Mutura
Umepakuliwa mara 916 | Umetazamwa mara 2,528
Download NotaJIFIKIRIE, WEWE USIPOINUKA! ( E.D.MUTURA)
Jifikirie, wewe usipoinuka na kwenda kutoa mchango wako, nani atalijenga Kanisa?x2
1. Inuka nenda katoe ulichonacho, tulijenge Kanisa letu; Usikubali kubaki katika kiti, twende tutoe tujenge Kanisa.
2. Kwa ukarimu wa kila mmoja wetu, tutalijenga Kanisa letu; Baraka za Mungu zitatutiririkia, twende tutoe tujenge Kanisa.
3. Usipotoa kwa moyo wa ukunjufu, utafukuza baraka za Mungu; Usibanie hata senti yoyote, Mungu mwenyewe anakufahamu.
4. Hatupotezi kwa kumtolea mungu, twende tutoe tujenge Kanisa; Bali twajiwekea hazina mbinguni, kwa kulijenga Kanisa letu.